Mnara wa taa wa Barra

Mnara wa taa wa Barra ni mnara wa taa wa pili kujengwa huko Barra kwenye mji wa Salvador, jimbo la Bahia, nchini Brazil. Mnara wa kwanza kwenye nafasi hii ulijengwa kwa udongo ulioshindiliwa, na ulikuwa mnara wa taa wa pili kujengwa Amerika, baada ya mnara wa zamani wa Jumba la Fribourg huko Recife. Mnara wa sasa ulijengwa mnamo mwaka 1839 na kutolewa na Dom Pedro II wa Brazil. Umejengwa kwa uashi na kupakwa rangi kwa bendi nyeusi na nyeupe. Mnara wa taa una mrefu wa mita 22 na taa yake iya mwaka 1890 ina lenzi ya Fresnel. Mnara huu lijengwa ndani ya ngome iliyolinda mdomo wa bandari. Ngome pamoja na mnara wa taa ziliorodheshwa kama miundo ya kihistoria na Taasisi ya Urithi wa Kihistoria na Usanii mnamo mwaka1938


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Tubidy